February 26, 2019



KOCHA Mkuu wa Azam FC, Abdul Mingange jana ameongoza kikosi chake kwa mara ya kwanza na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 mbele ya Rhino Rangers kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho.

Mingange ametwaa mikoba ya aliyekuwa kocha mkuu Hans Pluijm na msaidizi wake Juma Mwambusi baada ya uongozi kuamua kuwatimua kwa kile walichoeleza ni matokeo mabaya ya Ligi Kuu Bara.

Mabao ya Azam FC yalifungwa na Tafadzwa Kutinyu aliyecheka na nyavu mara mbili ikiwa ni dakika ya 21 na 54 huku bao la tatu likiwekwa kimiani na Obrey Chirwa dakika ya 69.

Kwa matokeo hayo Azam FC wanatinga hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho ambalo kwa sasa halina bingwa mtetezi kwani Mtibwa Sugar alivuliwa ubingwa na KMC. 

4 COMMENTS:

  1. Replies
    1. Daraja la kwanza wanacheza kwa kutumia matako au mashujaa walikuwa pemium league

      Delete
    2. LUGHA JAMANI, MATAKO YANAKUJAJE HAPA? HUTAKI WENGINE WAWE NA MAWAZO YAO TOFAUTI NA YA KWAKO? TUJIFUNZE KUVUMILIANA INAFURAHISHA TUKIWA NA FORUM YA KUSOMA MAWAZO MBALIMBALI YA WATU BILA MATUSI WALA HISIA ZA CHUKI, UJUE WOTE WANAYO HAKI SAWA NA WEWE TU.

      Delete
  2. SIFA NI PALE AZAM ITAPOKUTANA NA YANGA NA SIMBA KWENYE LIGI MICHEZO ILIYOBAKI NA ITOKEE AZAM IKASHINDA. HAPO CHECHE ANAWEZA KUJIPA SIFA ANAZOZITAKA. PENDA TUSIPENDE PLUIJM NI KOCHA MZURI HAYA YANAYOTOKEA NI AJALI ZA MAKOCHA.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic