February 9, 2019


MENEJA wa timu ya Manchester United  Ole Gunnar Solskjaer amekubaliana na mipango ya bodi ya timu kubana matumizi kwa ajili ya usajili ili kutotumia pesa nyingi kwa ajili ya kutafuta saini ya wachezaji wenye majina makubwa.

United imetumia pesa nyingi kwenye usajili tangu kujiuzulu kwa Sir Alex Ferguson mwaka 2013 kwa kuwasajili Di Maria, Radamel Falcao, Alex Sanchez na Paul Pogba ambao walijiunga na timu hiyo kwa ada kubwa.

Meneja Solskjaer amesema haijalishi ukubwa wa jina kwenye thamani ya mchezaji ni lazima awe mmoja ambaye yupo fiti na chaguo sahihi. Mtu ambaye atakuwa kuwa nasi moja kwa moja ndani ya timu.

"Kuhusu kuwanunua wachezaji wenye majina hilo ni lazima tulidhibiti kwa kuwa kwa sasa tunapambana ili kufanikiwa kuwa kwenye nne bora pamoja na kuwa mabingwa, kama utawaangalia wachezaji, miaka yao bado ni vijana na kila siku wanaendelea kupambana.

"Tunahitaji wachezaji wenye uzoefu ambao watakaa na wachezaji kwa muda na wenye uwezo wa kuwa viongozi halisi kama ilivyo kwa Paul Pogba yupo katika umri ambao tunatarajia atabeba majukumu mengi ndani ya timu," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic