LICHA YA KUWEPO KWENYE ORODHA YA KIKOSI, KIUNGO SIMBA AEPUSHA TIMU KUPOKWA POINTI 3
KIUNGO Hassani Dilunga juzi aliwaweka matatani Simba baada ya kuingia uwanjani na kupasha kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya mwadui FC.
Kiungo huyo, juzi alikuwepo kwenye orodha ya wachezaji watakaoanzia benchi kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambao ulimalizika kwa Simba kushinda mabao 3-0.
Dilunga, licha ya kuwemo kwenye orodha hiyo, alifanya mazoezi ya awali kabla ya mechi lakini hakukaa benchi wakati timu hizo zilipomaliza kufanya mazoezi.
Kama angekalia tu benchi, maana yake angehesabika ametumika katika mchezo huo, lakini inaonekana Simba walishtuka mapema.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumamosi, uwanjani ni kuwa viongozi hao walishtukia kuwa kiungo huyo bado ana adhabu ya kusimamishwa mechi tatu na faini ya 500,000 na kufikia maamuzi ya kumuondoa kikosini haraka.
Dilunga alipewa adhabu hiyo na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), maarufu kama Kamati ya Saa 72 pamoja na beki wa Lipuli FC ya Iringa, Ibrahim Job kwa kosa la kuchelewa kuondoka uwanjani baada ya kukamilika kwa dakika za kipindi cha kwanza.
Tukio hilo lilitokea katika mchezo wa ligi kati ya timu hizo Novemba 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar uliomalizika kwa suluhu baada ya wachezaji hao kutegeana kutoka uwanjani baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.
Kiungo huyo, katika mchezo na Mwadui alikuwa ametimiza michezo mitatu kabla ya kuondolewa kikosini na kupelekwa jukwaani baada ya kuikosa mechi dhidi ya KMC pamoja na Singida United.
CHANZO: CHAMPIONI
MENEJA WA SIMBA UMEKOSA UMAKINI NI HATARI SANA WEKENI VIZURI KUMBUKUMBU ZA KADI ZOTE
ReplyDeleteKweli wachezaji was kibongo ni shida,sawa meneja anahusika lakini mhusika mkuu no dilunga,inamaana hakujua anatakiwa kutocheza mechi ngapi?au n mamluki
ReplyDeleteNI KWELI KABISA UNAYOSEMA MCHEZAJI MWENYEWE AWE MTU WA KWANZA KUTAMBUA ANA KADI AU HANA
DeleteNA MENEJA UNAJIONGEZA MBALI YA KADI WALIZONAZO WACHEZAJI WA TIMU YAKO, UNAWEKA KUMBUKUMBU PIA YA WACHEZAJI WENYE KADI WA TIMU NYINGINE ZOTE ILI UWE NA USHAHIDI WAKATI UKIFIKA WA KUWEKEANA PINGAMIZI UKISUBIRI KUMBUKUMBU ZA TFF UJUE IMEKULA KWENU
Delete