February 19, 2019


UONGOZI wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba umesema kuwa umejipanga kubeba pointi tatu katika mchezo wa leo utakaochezwa Uwanja wa Amri Abeid.

African Lyon wataikaribisha Simba leo majira ya saa 10:00 Jioni mchezo ambao utarushwa pia kwenye king'amuzi cha Azam TV.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kikosi kimejiaandaa kwa ajili ya mchezo huo na matumaini makubwa ni kuona wanaweza kupata pointi tatu.

"Tunawaheshimu African Lyon ni timu nzuri, ila nasi pia hatuna budi kufanya kile ambacho mashabiki wanahitaji, tayari wachezaji na uongozi umeweza kuimudu hali ya hewa ya huku Arusha, ni wakati tu, sapoti ya mashabiki pamoja na dua ni vitu muhimu," amesema Manara.

Simba ikimaliza mchezo wa leo itakuwa na kibarua kingine mbele dhidi ya Azam FC mchezo utakaochezwa Ijumaa Uwanja wa Taifa majira ya saa 10:00 Jioni vyote vikiwa ni viporo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic