KOCHA wa Tanzania Prisons, Adolf Richard amesema kuwa anatambua ugumu wa mchezo wao unaofuata dhidi ya Mbeya City ila hana hofu ana imani ataibuka na ushindi.
Prisons ilianza msimu kwa kuchechemea ila kwa sasa imeanza kurejesha matumaini kwa mashabiki wake kutokana na kupata matokeo katika mechi zake za karibuni ikiwa ni pamoja na kubeba pointi tatu mbele ya Azam FC.
"Ni mchezo mgumu kwetu hasa ukizingatia wote tupo kwenye mazingira ambayo tumeyazoea, hakuna haja ya kuwa na hofu katika hili tumejipanga na tunajua kile ambacho tutakifanya uwanjani, mashabiki watupe sapoti," amesema Richard.
Mbeya City wataikaribisha Prisons uwanja wa Sokoine, Jumatano ya Februari 20 mchezo utakaochezwa saa 10;00 jioni.
0 COMMENTS:
Post a Comment