February 24, 2019


KIKOSI cha Singida United, jana kiliibuka na ushindi wa bao moja mbele ya Coastal Union ya Tanga uliochezwa uwanja wa Chamazi na kutinga robo fainali kimaajabuajabu.

Bao pekee lililoipa ushindi Singida United ni lile la kujifunga mchezaji wa Coastal Union Kennedy Mpepe dakika ya tano kipindi cha kwanza ambalo lilidumu mpaka mwamuzi anakamilisha dakika 90 za mchezo.

Ushindi huo unamaanisha bado tatizo la safu ya ushambuliaji kwa kikosi cha Singida United ambalo kocha mkuu, Dragan Popadic amekuwa akizungumza mara nyingi halijatibika kisawasawa.

Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema bado wanajipanga kuona wanatimiza lengo la kubeba kombe la FA kibabe msimu huu kama ambavyo walileta ushindani mwaka jana kwa kutinga fainali,

Katika matokeo mengine ya jana , Kagera Sugar aliibuka mbabe mbele ya Boma FC kwa ushindi wa mabao 2-1.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic