February 24, 2019




IMEELEZWA kuwa baada ya Azam FC kuachana rasmi na aliyekuwa kocha mkuu, Hans Pluijm pamoja na msaidizi wake Juma Mwambusi nafasi zao zitazibwa kwa muda na makocha wa timu za vijana.

Maamuzi hayo ya haraka yamekuja kwa makubaliano ya pande zote mbili kukubaliana kutokana na kutoridhishwa na matokeo yake ya hivi karibuni ya kwenye mechi za Ligi Kuu Bara (TPL).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu ya Azam FC, sasa benchi la ufundi litakuwa chini ya makocha wa timu za vijana, Meja Mstaafu Abdul Mingange (U20) na Idd Cheche (U17).

Pia kwa sasa uongozi wa Azam tayari umeanza mchakato wa kumtafuta atakayerithi mikoba ya kocha huyo raia wa Uholanzi.

Pluijm ameiongoza Azam FC kwenye michezo 25 na amepoteza michezo mitatu ameshinda 14 na kutoa sare nane akiwa na pointi 50 nafasi ya pili.

Michezo yake ya hivi karibuni kubanwa mbavu ilikuwa dhidi ya Alliance FC ambao alitoas sare (1-1), Lipuli pia alitoa sare(1-1) kabla ya kupoteza kwa Tanzania Prisons(1-0)  na kutoa sare kwa Coastal Union (1-1) na kumalizia kichapo kutoka kwa Simba (3-1).

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic