February 22, 2019


MOTO wa Ligi Kuu Bara unaendelea kushika kasi ikiwa kwa sasa ni mzunguko wa pili ambao huamua nani awe bingwa na nani atashuka daraja.

Mpaka sasa hakuna aliyejihakikishia ubingwa kutokana na uwepo wa ile kauli ya shinda mechi zako nami nishinde zangu huku ushindani mkubwa ukiwa ni kwa Yanga, Azam na Simba ambao wanashika nafasi tatu za juu.

Hali kwa timu mbili ambazo zimepanda daraja msimuu huu sio nzuri kwani zinaonekana zikipumulia mashine kutokana na matokeo ambayo wanayapata kwa sasa.

Kipigo cha mabao 2-1 ilichokipata Biashara United mbele ya Mwadui kimeifanya Bisahara United kubaki na ponti 23 huku ikiwa imecheza michezo 26 na inashika nafasi ya 19.

African Lyon nao mambo bado si shwari baada ya kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Simba kumeifanya iwe nafasi ya 20 baada ya kucheza mechi 27 ikiwa na pointi 21.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic