February 22, 2019



LEO saa 10:00 jioni, Uwanja wa Mkapa nyasi zitawaka moto kwa kuwakutanisha mafahari wawili ambao vita yao kubwa ni kuishusha Yanga kileleni.

Huu ni mchezo wa kwanza kwa wapinzani hawa kukutana msimu huu wa mwaka 2018/19 huku mwenyeji wa mchezo akiwa ni Azam FC.

Mpaka sasa tangu Azam FC ipande daraja msimu wa mwaka 2013/14 na kushiriki Ligi Kuu Bara imekutana na Simba mara 10.

Katika michezo yote hiyo hakuna mbabe hata mmoja ambaye ameweza kumuonea mwenzake kwa kumfunga mabao mengi zaidi wote wameishia kufungana mabao 2 ama bao moja.

Wote wawili wametoa sare mara nne na kila mmoja ameshinda  mara tatu hali ambayo inaonyesha ushindani ni mkubwa zinapokutana timu hizi.

Zilipokutana kwenye mismu yao mitano iliyopita Ligi Kuu Bara matokeo yao yalikuwa hivi:-

2013/14
Simba 1-2 Azam FC
Azam FC 2-1 Simba

2014/15
Azam FC 1-1 Simba
Simba 2-1 Azam FC

2015/16
Azam FC 2-2 Simba
Simba 0-0 Azam FC

2016/17
Azam FC 0-1 Simba
Simba 0-1 Azam FC

2017/18
Simba 1-0 Azam
Azam 0-0 Simba

2018/19 ?

Leo ndo atajulikana nani mbabe ambaye ataanza safari ya kumkibiza kinara Yanga mwenye pointi 61, Azam wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 50, Simba nafasi ya tatu pointi 42.

1 COMMENTS:

  1. Hebu fanyeni tafiti kabla hamja toa hizo takwimu zenu. Unataka kuniaminisha kua Azam alipanda daraja na kua bingwa msimu huohuo? Maana 2013-14 Azam ndo alikua bingwa was vpl
    chini ya kocha Joseph Omog.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic