Kamati hiyo imekuja mara baada ya viongozi Samuel Lukumay aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga sambamba na Hussein Nyika aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Usajili na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji kutangaza kujiuzulu.
Kamati hiyo ya muda ambayo itaiongoza klabu ya Yanga kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo uliopangwa kufanyika Jumapili ya Aprili 28 , 2019.
Kamati zilizochaguliwa ni mbili ambapo kuna kamati ya uchaguzi ya Yanga na kamati ya muda ya kufikisha Yanga kwenye Uchaguzi Mkuu.
Kamati mpya ya Uchaguzi itakuwa chini ya Mwanasheria Samuel Mapande ambaye atakuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo huku wajumbe Daniel Mlewa, Mustapha Nagali, Godfrey Mapunda, Edward Mwakingwe, Samuel Mangesho, Issa Gavu, Venance Mwamoto, Seif Gulamali na Dastan Kitandula.
Mbali na uchaguzi, walioteuliwa kwenye Kamati ya Utendaji kwa muda ni Mwenyekiti wa Kamati Lucas Mashauri, Makamu Mwenyekiti Mussa Ntimizi (Mbunge Igalula).
Wajumbe ni Hussein Nyika, Hussein Ndama, Moses Katabaro na Samuel Lucumay pamoja na Maulid Kitenge.
Wakati Kamati hizo zikitangazwa, uchaguzi wa klabu hiyo umepangwa kufanyika tarehe 28 April 2019.








0 COMMENTS:
Post a Comment