March 27, 2019


MOHAMED Rashid ameonesha cheche zake leo kwenye mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya African Lyon baada ya kufunga bao la kuongza kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.

Mo Rashid alitumia dakika moja na nusu kipindi cha pili baada ya dakika 45 za kwanza kukamilika bila kufungana ndipo dakika ya 46 na sekunde 30 akamalizia pasi ya Omary Ramadhan akiwa nje ya 18 na kuujaza mpira wavuni kwa guu lake la kulia.



Dakika ya 88 Cllif Buyoya alimaliza karata ya mwisho kwa kupachika bao la pili kwa guu lake la kulia akimaliza pasi ya Omary Ramadhan na kuifanya Lyon kushindwa kuwa na makali kwenye mchezo huo wa hatua ya robo fainali.

KMC wanatiga nusu fainali huku wakimsubiri mshindi kati ya mchezo wa Kagera Sugar na Azam FC utakaochezwa Uwanja wa Kaitaba Ijumaa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic