March 27, 2019


HARUNA Shamte, mshambuliaji wa Lipuli, amewatungua bao la Usiku Singida United lililowamaliza nguvu wapinzani yao kupambana katika mchezo wa leo wa hatua ya robo fainali wa kombe la Shirikisho uliochezwa Uwanja wa Samora.

Shamte alimaliza hesabu dakika ya 90 kwa mpira uliokufa baada ya Jimmy Shoji kufungulia milango dakika ya 33 kwa guu lake la kushoto akimalizia pasi ya Paul Nonga.

Singida United msimu uliopita walitinga hatua ya fainali ambapo walitunguliwa mabao 2-1 na Mtibwa Sugar ambao walitwaa ubingwa.

Kwa sasa Lipuli wanamsubiri mshindi kati ya Alliance ama Yanga ambao watacheza machi 31 Uwanja wa CCM Kirumba ili kumenyana hatua ya nusu fainali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic