March 26, 2019


Na George Mganga

Mchezaji wa klabu ya Simba, Shomari Kapombe, amesema kuwa hali yake inaendelea vizuri kwa sasa kutokana na majeruhi aliyoyapata wakati akiwa na kikosi cha Taifa Stars.

Kwa mujibu wa Radio EFM, Kapombe aliumia mguu kwa kuvunjika mfupa wa ndani huko Afrika Kusini wakati kikosi cha Stars kilipokuwa kimeweka kambi maalum kujiandaa na mechi za kuwania kufuzu AFCON dhidi ya Lesotho.

Baada ya matibabu kukamilika Kapombe ameeleza kwa sasa maendeleo yake ni mazuri na tayari ameshaanza mazoezi mepesi nje ya uwanja huku akisema anatarajia kuanza kujifua na timu yake ya Simba mwishoni mwa mwezi huu.

"Namshukuru Mungu hali yangu kwa sasa inaendelea vizuri.

"Natarajia kuanza mazoezi mepesi na wachezaji wenzangu mwishoni mwa mwezi huu.

Kuhusu Taifa Stars kufuzu kuingia kwenye mashindano ya AFCON mwaka huu yatakayofanyika huko Misri kwa kuifunga Uganda mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Kapombe amefunguka akieleza kufurahia na akiwapongeza wote waliofanikisha hilo.

"Nimefurahi sana kama mtanzania ambaye pia nilikuwa kwenye kikosi huko nyuma licha ya kutolewa baadaye kwakuwa nisingeweza kucheza.

"Natoa pongezi kubwa kwa wachezaji wenzangu, na wale waliosaidia kufika hatua hii.

"Kwakweli ni jambo kubwa sana kutokea kwasababu ni miaka 39 nafasi hii ilikuwa haijatokea kwetu, nina furaha kubwa kwakweli".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic