KOCHA wa kikosi cha Mbao FC, Salum Mayanga anaanza na mtihani mzito kwenye kikosi chake kutokana na kukutana na timu ambayo ipo moto kwenye ligi na ina hasira ya kupoteza mchezo wake wa kwanza uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba kwa kufungwa bao 1-0.
Simba itamenyana na Mbao Machi 31 Uwanja wa CCM Kirumba baada ya Uwanja wa Taifa kuwa kwenye marekebisho, huku Simba tayari wameonja utamu wa kutinga hatua ya robo fainali baada ya kuwatungua AS Vita mabao 2-1.
Kocha wa Simba, Patrick Aussems amesema baada ya kikosi chake kufuzu hatua ya robo fainali hesabu zake ni kuona anapata matokeo kwenye mechi zake zinazofuata za ligi kuu licha ya ratiba kumbana.
"Natambua nina michezo mingi ambayo natakiwa kucheza kwa sasa kwenye ligi ila hilo litanifanya niwe kwenye mpangilio mgumu wa ratiba pamoja na wachezaji kuona namna gani nitawagawa ila hainipi shinda ninaamini wachezaji wangu wote wana uwezo wa kunipa matokeo.
"Hakuna timu ambayo ni ndogo kwenye ligi kuu hata Mbeya City, Lipuli, Mbao ni timu kubwa lakini mimi ninachotaka ni matokeo na nimewaambia wachezaji wangu hakuna cha kupoteza kwa sasa tunahitaji ushindi," amesema Aussems.







0 COMMENTS:
Post a Comment