March 27, 2019


UONGOZI wa timu ya KMC umesema kuwa upo tayari kwa mchezo wao wa leo dhidi ya African Lyon ambao ni wa kombe la Shirikisho utakaopigwa Uwanja wa Isamuhyo  huku hesabu zao zikiwa ni kupata matokeo chanya mbele ya wapinzani wao.

Ofisa Habari wa KMC, Anwari Binde amesema kuwa wanaingia kwenye mchezo wa leo kwa tahadhari kubwa kutokana na hatua ya robo fainali kuwa ya mtoano huku wakitambua wapinzani wao hawana mchezo kwenye kombe hili.

"Tahadhari kubwa tunachukua ukizingatia kwamba wapinzani wetu ligi kuu hawafanyi vizuri hivyo nguvu zao zote wataziweka huku ili kupenya.

"Tunawaheshimu hilo lipo wazi ila tunahitaji matokeo ili kusonga mbele na hatimaye kubeba kombe ambalo kwa sasa ndio hesabu zetu kuona tunaanza kujaza makabati kwani tayari tumejipanga kulichonga," amesema Binde.

Kombe hili pia linapigiwa hesabu kwa ukaribu na kikosi cha Yanga ambacho kipo chini ya kocha Mwinyi Zahera ambaye hivi karibuni alisema kuwa atapambana kulibeba kombe hilo ili timu iwe ya kimataifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic