March 27, 2019


Katika kuhakikisha kikosi cha Simba kinafanya vizuri kwa kuwekwa hamasa ya nguvu, unaambiwa mabosi wa timu hiyo wamemnunulia gari mpya Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems.

Gari hilo ambalo ni aina ya Toyota Wish, Aussems ameanza kulitumia jana wakati kikosi cha Simba kikijifua kwenye Uwanja wa Bocco Veterani kwa ajili ya mechi zijazo za ligi.

Awali Kocha huyo alikuwa akitumia gari ambayo ilikuwa inatumiwa na Makocha waliopita akiwemo Joseph Omog, Jackson Mayanja na Pierre Lechantre.

Taarifa zinasema Aussems aliomba kubadilishiwa ndiga hiyo ili aweze kutimiza majukumu yake ya kazi vizuri na kwa ufasaha zaidi.

Wakati huo kikosi cha Simba kinaendelea kujiandaa na mechi ya ligi ambapo wikiendi ijayo kitakuwa na mchezo dhidi ya Mbao FC, mechi ikipigwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.





1 COMMENTS:

  1. yaani toyota wish nayo ni habari!!! Nyie mmeishiwa kweli!!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic