March 21, 2019


MWENYEKITI wa Kamati ya Uhamasishaji kuelekea mchezo wa ya Taifa Stars kufuzu michuano ya AFCON dhidi ya timu ya taifa ya Uganda, ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  ameshukuru mwitikio wa Watanzania ambao wamekuwa wakiisapoti timu hiyo na kuwataka wajitokeze kwa wingi kuishabikia ili ishinde na kutinga michuano hiyo.

Amesema hayo leo Alhamisi, Machi 21, 2019 wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, na kuwashukuru watu wote wanaotoa tiketi za bure kwa Watanzania kwenda uwanjani kuishangilia Taifa Stars Jumapili ijayo.

“Ninatoa ruhusa kwa daladala yoyote kutoka sehemu yoyote ya jiji la Dar, siku hiyo waendeshe route (njia) ya kutoka popote walipo kwenda Uwanja wa Taifa. Ukipata shida yoyote njiani nitafute mimi. Tukishinda mechi hii nitakahikikisha tunafanya party (karamu) kubwa sana ndani ya hili jiji la Dar na Tanzania kwa jumla.

“Leo asubuhi nimeongea na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, na amekubali kuwa mgeni rasmi wa mchezo huo. Kazi yangu kama mwenyekiti wa kamati hii ni kuiweka timu mikononi mwa Watanzania. Nashukuru media (vyombo vya habari) zote kwa kutuunga mkono kazi yetu.  Ninaamini timu hii ipo mikononi mwa Tanzania rasmi. Twendeni uwanjani,” amesema Makonda.

3 COMMENTS:

  1. Muheshimiwa mkuu wa mkoa yupo sahihi katika kuhimiza ushindi ila wakati mwengine TFF lazima wajitafakari kwenye baadhi ya maamuzi yao. Muheshimiwa rahisi Magufuli aliwapa Simba maelekezo ya maneno mara moja tu na utekelezaji wa maagizo hayo kwa Simba na viongozi wake kwa kiasi fulani wameyafanyia kazi sihaba.Maagizo ya Magufuli kwa Simba kiuhalisia hayakuwa kwa ajili ya Simba peke yao bali kwa taasisi zote za michezo nchini.Jambo la kwanza kwenye eneo waliloanzia kulifanyia kazi Simba kwa umakini ni utafutwaji wa kocha makini na mwenye uwezo. Kwenye mpira wa miguu uwezo wa kocha katika kuwaandaa wachezaji wake katika upatikanaji wa ushindi ni sawa na uwezo wa mwalimu darasani shuleni. Hata shule iwe na majengo mazuri kiasi gani kama mwalimu hajui anachokifanya basi ni kazi bure.Dunia ya sasa mambo yanaenda au kuendeshwa kwa kasi ya ajabu katika shghuli za kila siku na sisi watanzania hasa viongozi kama wanafamilia wa Dunia hii basi hatuna budi ya kubadilika au kuadapt hali hiyo ili kuendana na mwendo kasi kazi wa dunia ya leo. Mamabo ya kusubiri mpaka tunalizwa ndio tufanye mabadiliko ya uongozi ni ujinga wa kujitakia. La kushangaza kwanini viongozi wetu wanashindwa kufauata nyayo za Magufuli katika utendaji wa kazi. Magufuli aliita timu ya Taifa ikulu na uanapoona kiongozi wa nchi amewaita watendaji wake ikulu hapo lazima kutakuwa kuna Jambo. Lakini Stars hawakuitwa tu bali Muheshimiwa raisi aliizawadia Taifa stars motisha wa pesa taslimu lakini kilichotokea kule lethoso kwa taifa stars hakuna haja ya kukisema tana hapa. Hakuna haja ya kumumunya maneno kwani mchezo wa mpira huchezwa hadharani na uwezo wa kocha wa Taifa stars Amunike hauendani kabisa na kiu na matarajio ya watanzania wengi kuiona timu yao ya Taifa ikifanya vizuri. Mfano As vita walilalamikia baadhi ya mambo nje ya uwanja lakini hawakuwa na mashaka hata kidogo juu ya uwezo wa Simba uwanjani . Tukija kwa uwezo wa kocha wa Taifa stars na majukumu aliyopewa ni dhahiri kocha huyo amepewa kichwa cha muendawazimu kujifundishia konyoa.Na kuelekea mechi ya kufuzu Afcon jumapili watanzania tutgemee zaidi huruma ya waganda jinsi watakavyoikabili taifa stars. Lakini kiuwezo waganda wanauwezo wa kututandika hapahapa kwetu nyumbani hilo halina shaka shukrani kwa viongozi wa soka wa Uganda kwa usaili makini uliopelekea timu yao ya taifa kuwa na Kocha mwenye uwezo na anaejua kazi yake .Kocha wa stars alianza kazi yake na staili ya Jose Marihno ya kuanzisha figisu na wachezaji na sidhani kama mwanzo mzuri kwa afya ya taifa stars.

    ReplyDelete
  2. Wakat mwingne tupunguze kuongea sana kwenye media km kamati naamin walichowaahid wachezaji ingebaki siri kdogo mtawafanya waganda waje wamejiandaa kutukazia asee bro DAB punguza kick kwny media basi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic