MAKONDA AITISHA KIKAO NA WANAMICHEZO LEO, AZUNGUMZIA SUALA LA KAPOMBE STARS
Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Saidia Taifa Stars ishinde na Mkuu wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema leo majira ya saa sita watakuwa na kikao na wanahari kwa ajili kutoa dira nzima ya Taifa Stars kutokana na furaha waliyonayo juu ya kufuzu AFCON.
Stars ilifanikiwa kufuzu kwa kuichapa Uganda jumla ya mabao 3-0 kwenye mchezo uliofanyika jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Taifa Jumapili iliyopita.
Akizungumza na Radio EFM, Makonda amefunguka kuwa furaha aliyonayo ni kubwa na leo watazungumza mengi katika Hotel ya Serena iliyopo katikakati ya jiji la Dar es Salaam.
Mbali na kuitisha kikao hicho, Makonda amezungumzia pia suala la wachezaji ambao hawakuhusika katika mchezo wa mwisho wa Stars dhidi ya Uganda ikiwemo Shomari Kapombe aliyeumia Afrika Kusini.
Makonda amesema suala hilo linaweza kujadiliwa zaidi na Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo kupitia Waziri wake Harrison Mwakyembe pamoja na Naibu wake, Juliana Shonza.
Makonda amefunguka kuwa yeye alikuwa kwenye kamati maalumu ya kuisaidia Stars ishinde kwa ajili ya kufuzu AFCON ambayo itafanyika huko Misri japo akieleza pia hakuna kilichoharibika na anatambua wachezaji wote waliokuwa kwenye kikosi cha Stars watakuwa na furaha.








Nimkumbushe mheshimiwa tu kwamba kama ile mechi ingekuwa ndiyo fainali ya AFCON , Shomari Kapombe angepewa medali ya mshindi hivyo nadhani ana haki ya kujumuishwa kwenye faida na zawadi kama walivyopewa wenzake maana mechi ya juzi isingefikiwa kama ushindi wa awali aliouchangia usingekuwepo. NA YEYE APEWE ZAWADI NI MTANZANIA MZALENDO.
ReplyDelete