UONGOZI wa Singida United umesema kuwa umejipanga kuwanyoosha wapinzani wao Lipuli kwenye mchezo wao wa hatua ya robo fainali utakaochezwa kesho Uwanja wa Samora.
Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa kikosi kimejipanga na morali ni kubwa kikiwa chini ya kocha Fred Minziro 'Baba Isaya'.
"Kwa sasa moto wa kikosi ni mkubwa na wachezaji wana morali kwani mpaka sasa zile kelele ndani ya timu zimekwisha na kocha Baba Isaya anajua namna ya kuiendesha timu ukizingatia yeye aliipandisha kwenye ligi, hivyo Lipuli watatusamehe tutawanyoosha kivyovyote vile.
"Tuna uzoefu na mashindano haya na tulifika hatua ya fainali kwenye michuano hii, tutatumia uzoefu kupata matokeo kwenye mchezo wetu, kikubwa ni sapoti ya mashabiki kuona namna tutakavyopata matokeo ugenini," amesema Katemana.








0 COMMENTS:
Post a Comment