MBAO FC waliitungua Simba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, wamepania kuivuruga Simba kwenye mchezo wao wa Jumapili utakaochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Mbao kwa sasa ipo nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza michezo 30 ikiwa imejikusanyia pointi 36 itamenyana na Simba ambayo ipo nafasi ya tatu baada ya kucheza michezo 21 ikiwa na pointi 54.
Kocha Mkuu wa Mbao, Salum Mayanga amesema "Tunajua tunakwenda kukutana na timu ya aina gani hivyo hatuna mashaka lazima tutapambana kutafuta matokeo uwanjani, tuna mipango mikali.
"Maandalizi yetu yamekamilika hivyo kilichobaki kwa sasa ni kuona namna gani mchezo utakuwa ndani ya dakika 90 ambazo zitaamua matokeo, mashabiki wajitokeze kutupa sapoti," amesema Mayanga.







Lazima.ukumbuke kuwa Simba ya leo siyo kabisa ile mlioifunga bao moja na kama husadiki nenda ukawsulize akina Lipuli, Ruvu shooting na Yanga waliojigamba watakwambia kilichowapata
ReplyDeleteMbao Msijindanganye Kabisa Kupata Tena Pointi 3 Kwa Simba Hii Tena Iliyo Tinga Robo Fainal Kwenye Club Bingwa Hata Hata Mkipewa Akina Salamba Mtafungwa Tu Zaidi Mjipange Kwa Mech Nyingine Zilizo Mbele Yenu
ReplyDeletehizi timu hazichelewi kuimba wimbo wao wa mapambio wakifungwa...."marefa wanaibeba Simba"...Kinachonishangaza unaporejea kwenye takwimu za mechi ilivyochezwa unakuta Simba possesion 70% na timu pinzani 30%.Sasa hapo Simba anakuwa anabebwaje?Makocha wetu wazawa mjitathimini bana tumeshawachoka na nyimbo zenu za mapambio ya marefarii.
ReplyDelete