March 24, 2019


MSHAMBULIAJI wa timu ya Simba, Meddie Kagere amesema kwa sasa kazi kubwa kwao ni kuendeleza furaha ndani ya kikosi cha Simba kwa kupata matokeo chanya yatakayofanya wafikie malengo waliyojiwekea.

Kagere amesema kuwa ushindani uliopo kwenye ligi ni mkubwa na kila timu inapigia hesabu kupata matokeo uwanjani.

"Kila timu imejipanga kupata matokeo hicho ndicho tulichonacho sisi pia, tunatambua kwamba aliye juu yetu alishinda mechi zake hivyo kazi yetu pia ni moja kushinda mechi, mashabiki watupe sapoti ili tufanye vizuri," amesema Kagere.

Kagere kwa sasa anashika nafasi ya pili kwa kutupia mabao kwenye ligi ambapo mpaka sasa ametupia mabao 13 huku kinara kwa utupiaji ni Salim Aiyee wa Mwadui FC mwenye mabao 16.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic