BEHEWA Sembwana aliyekuwa kiungo wa Kagera Sugar amefariki dunia leo alfajiri kutokana na kuugua tumbo.
Kiungo huyo amesumbuliwa na maumivu ya tumbo kwa muda mrefu, hali ambayo ilimlazimu kufanyiwa opereshe zaidi ya mara mbili katika hospitali tofauti.
Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema ni pigo kwao kumpoteza mchezaji wao ambaye alikuwa bado kijana na ana uwezo mkubwa ila kazi ya Mungu haina makosa.
“Tatizo lake lilikuwa ni tumbo kwani amekuwa akisumbuliwa na tumbo licha ya kampuni kujitahidi kumpa huduma kwa kumpeleka hospitali kupewa matibabu bado alikuwa akipata nafuu na maumivu yanarejea tena.
"Alifanywa upasuaji zaidi ya mara mbili na kampuni ilianza kumpeleka hospitali ya Bukoba kabla ya kumpeleka Bungado na baadaye kumhamishia Muhimbili, mapenzi ya Mungu yametia hivyo tumuombee kheri," amesema Maxime.
0 COMMENTS:
Post a Comment