BODI ya Udhamini ya Klabu ya Yanga leo imeteua Kamati mpya ya Mashindano itakayosimamia mechi za Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho.
Hiyo, ikiwa ni saa chache tangu aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa timu hiyo, Samuel Luckumay na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mashindano ya timu hiyo, Husseni Nyika kutangaza kujiudhuru.
Akizungumza kwenye Makao Makuu ya Klabu hiyo Jangwani jijini Dar es Salaam, Waziri, George Mkuchika alisema kamati itafanyakazi yake kwa muda wa mwezi mmoja pekee ambayo itavunjika baada ya Uchaguzi Mkuu wa Yanga kufanyika Aprili 28, mwaka huu.
Mkuchika aliitaja kamati hiyo itakayoongozwa na Mwenyekiti wake Lucas Mashauri Makamu wake, Said Ntimizi Wajumbe ni Samwel Lukumay, Hussein Nyika, Katabalo, Ndama na Maulid Kitenge.








Kwani huyu si ndo alituambia Manji anarudi ofisini Sasa imekuwaje tena
ReplyDelete