March 22, 2019


Baada ya Simba kupangwa kucheza na TP Mazembe katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Mwenyekiti wa zamani wa timu hiyo, Ismail Aden Rage, amesema Mazembe kwa sasa ni jina tu.

Rage ameeleza kuwa Mazembe kali aliyokuwa anaifahamu ni ile iliyokuwa na wachezaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu na si hii ya sasa.

Amesema kipindi ina watanzania hao wawili ilikuwa na moto wa kuotea mbali tofauti na ya sasa ambayo itakuwa mchekea kwa Simba.

"Niwaondoe hofu wanasimba wote, Mazembe ya sasa imebaki jina tu.

"Mazembe iliyokuwa na Samatta pamoja na Ulimwengu ndiyo ilikuwa na balaa lake.

"Hivyo Simba tunapaswa nafasi ya kufuzu kwenda nusu fainali, kwangu naamini tutashinda wala hakuna wasiwasi".

Simba itakutana na Mazembe Aprili 5/6 katika mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaam na baadaye Simba watasafiri kuelekea Lubumbashi kurudiana nao 12/13 Aprili huko Congo.

4 COMMENTS:

  1. Huu ndo ujinga wa Watanzania siku zote kujiaminisha maji ya mto ni mafupi kwa sababu ya kuangalia kiangazi kilichopo.Rage usitudanganye huenda utakuwa umetumwa utuuze

    ReplyDelete
  2. Anachoongea Rage kinaukweli kiasi chake nimewaangalia Mazembe mechi kadhaa hawana speed sana kama Mazembe Ile ya akina Samatta. Ila ni timu nzuri na ni timu kuwa MFUMO wa uchezaji wa sasa wa TP sio sababu ya kuwadharau bado ni timu hatari

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unapoingia vitani hutakiwi kumdharau adui kwa hali yoyote ile,unatakiwa kupambana naye bila kujali udhaifu wake hata kama unaujua na ndo maana ukikuta hata kichaka unakisambaratisha ukiamini ni ngome ya adui

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic