MADARAKA SULEIMAN AWAPA SIMBA DAWA YA KUWAMALIZA MAZEMBE
Mchezaji wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Madaraka Suleiman, amewapa mbinu Simba za kuhakikisha wanaboresha safu ya ulinzi ili kujiwekea nafasi ya kufanya vizuri katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe.
Suleiman amesema hayo kutokana na safu ya Simba kuonesha mapungufu hayo haswa ikiwa katika michezo ya ugenini jambo ambalo linaweza kugharimu.
Mkongwe huyo aliyeng'ara miaka hiyo, ameeleza kuwa mechi hiyo itakuwa ngumu kutokana na Mazembe kuwa na uzoefu wa muda mrefu katika mashindano ya kimataifa.
Amefunguka kwa kuwasisitiza Simba kuhakikisha safu ya ulinzi inaimarishwa vizuri kwa maana washambuliaji wa Mazembe wamekuwa na njaa ya kupata mabao.
Tmu hizo mbili zitakutana jijini Dar es Salaam katika mzunguko wa kwanza kabla ya Simba kwenda Lubumbashi, Congo kwenye mechi ya marudiano.
0 COMMENTS:
Post a Comment