SIMBA, AJIBU WAMALIZANA
YANGA SC waliwafanyia umafia Simba kwa kumng’oa Ibrahim Ajibu na kwenda kumtambulisha kwa mbwembwe kisha wakampa uzi wa kijani misimu miwili nyuma.
Simba wenyewe walijipoza machungu hayo kwa kumchomoa kiungo fundi Haruna Niyonzima na kumpa jezi nyekundu. Lakini taarifa ikufikie kwamba mara ligi itakapomalizika tu muda wowote Ajibu atarudi kule alikotoka kwa kuvaa tena jezi nyekundu.
Vigogo wa Simba wameamua kwani wanataka kuona kombinesheni ya Ajibu na Niyonzima pembeni wakiwa wanawalisha mipira tu washambuliaji wao wakiongozwa na Meddie Kagere.
Ishu iliyotufikia mezani ni kwamba tayari Simba wameshamalizana na nahodha huyo wa Yanga na kuna mkataba amesaini lakini ukiwa ni ule wa awali.
Nahodha huyo wa Yanga kwa sasa anahesabu tu siku ndani ya klabu yake hiyo kisha achukue virago vyake na kurudi kwao. Waswahili wanasema nyumbani kumenoga. Mkataba wake unafika ukingoni pale msimu huu utakapogota mwishoni.
Habari ambazo Championi Jumatatu, limevujishiwa ni kwamba kila kitu juu ya Simba na kiungo huyo mwenye asisti 15 msimu huu kimeenda safi.
“Mkataba wake na Yanga unaisha mwisho wa msimu huu, hivyo kilichofanyika ni kumbeba juu kwa juu kabla mambo hayajawa mengi kwa sasa ndani ya Simba.
“Uongozi umeamua kujipanga kuongeza makali ndani ya Simba ili kufanya kikosi kuwa na nguvu na chenye ushindani, sasa njia ya kwanza ni kuwa na wachezaji wenye vipaji kama ilivyo kwa Ajibu,” kilieleza chanzo hicho.
Kwa mujibu wa Championi Jumatatu, linasema lilimbana Meneja wa Ajibu ambaye ni kaka yake, Athuman Ajibu juu ya ishu hiyo na kusema kuwa bado mchezaji wake ana mkataba na Yanga kwa sasa, hivyo itakuwa ngumu kuzungumzia hilo.
“Ajibu ni mali ya Yanga kwa sasa hivyo siwezi kusema yupo Simba na amesaini huko, hilo ni jambo gumu kulizungumzia,” alisema Athuman.
CHANZO: CHAMPIONI








Acha kumtafutia soko Ajib,Simba hawana haja na Ajib waowanaangalia mashindano ya CAF kwa mwaka ujao.
ReplyDeleteAjibu kabla ya kufikiria kurudi msimbazi tafuta suluhisho linolokufanya kushindwa kuitwa Taifa stars kwani Afcon inaweza kukuondosha Tanzania. Kwa upande wa Simba bado watanzania hatuamini macho yetu kinachoendelea kwa Adam Salamba? Kumbe vurugu zake zote zile akiwa Iringa ni kutaka kuja Dar halafu azimike zii? Kitendo cha Salamba hata kufikiriwa kuitwa timu ya Taifa ni Aibu kwa kijana na mchezaji alietarajiwa kufanya makubwa na watanzania wengi. Kuchezea timu ya Taifa hivi sasa ni big deal na mchezaji mwenye kujielewa kamwe hawezi kuzembea kutopata nafasi ya kuitwa kuitumikia. Kwa Salamba ingekuwa rahisi kwake kuitwa Taifa kama angeonyesha uwezo pale Simba. Kwa mchezaji yeyote atakaekujakupata nafasi ya kuitumikia taifa stars Afcon Misri basi inawezekana ikawa ndio ticket yake ya kuondoka Tanzania kwa kwa maslahi makubwa zaidi ya kikazi nje ya nchi ni vyema vijana kuonesha bidii ili kupata nafasi ya kuitwa Taifa stars kwani ni heshima kwa mchezaji pia.
ReplyDeleteKama Ajibu atakubali kurejea SimbaSCTanzania nadhani ndo utakuwa mmwisho wa kipaji chake..
ReplyDeleteAnashindwa nini kutafuta timu hata ndani ya nchi za Afrika Mashariki..??
Anyway; uongozi wa SimbaSCTanzania pia ni wavivu sana wa kufanya scouting.. Ajibu wa nini sasa pale kwenye kikosi chao..??
Au ndo zile commission mtu anatafuta pa kutokea amalizie mjengo wake au apate mtaji wa kabiashara kake..??
I do not see Ajibu has ability to play Simba Sport Club now. Ajibu did leave Simba Sport Club while the club was in need of him but he left as if he was overwhelmed but not. A such kind of players are not required. This what happened to Hassan Kessy.
ReplyDeleteSimba as a club has to conduct enough scouting before calling any players. This is very Important.
jackbertha@gmail.com
Mpira Wa Tanzania unatabilika sana mfano ni hotuba ya mh.mstaafu rais jakaya kikwete chezaji hata km huna matumizi nae lakin akikusumbua tu unamnunua na kuaribu kipaji chake ...ajibu akili kumkichwa kama unaitaji ela zaid nenda simba lakin km bado unaitaji kuimprove zaid kaa n zahera
ReplyDeleteUliishia darasa la ngapi wewe maana unashindwa hata kuandika Kiswahili fasaha
DeleteUmenena vizuri huyu Ajibu pale simba hana na hatapata namba kamwe, muda huu wa Niyonzima, dilunga, chama, rashid juma tu. Kama Mo ibrahimu ambae ni fundi kuliko Ajibu na ndiye aliyeanza kumpiga benchi pale simba kabla ya kutimkia Yanga naye anasugua benchi sembuse huyu Ajibu, hizi ni porojo tu
Deletembona mnamtaja sana ajibu? mnaweza onesha mkataba aliokwisha saini ajibu huko simba? kwa nini tunaishai kwa kudhania sana wakati siku hizi kila kitu kiko wazimkabisa, maisha ya mpira ni pesa kila mtu anaweza kuhamia popote anapotaka kwa maslahi yake,
ReplyDeleteAjibu kama unaona kuna hela unayoitaka nenda msimu ukimalizika huna sababu ya kubaki yanga kama dau wanalokupa ni dogo kuliko la simba au timu nyingine
Duh ama kweli mpira pesa...akili mkichwa.kama Ajib anataka sifa toka jukwaani na wapambe hawa waandishi wa habari aendelee tu kubaki Yanga.Lkn kama anataka mkwanja basi kwa nini asijiunge na Simba au na timu yoyote yenye mkwanja wa maana?Uamuzi unao mwenyewe Ajibu Migomba.
ReplyDelete