March 31, 2019


KIKOSI cha Simba kimeendelea na moto wake wa kumaliza viporo vya ligi kwa ushindi baada ya kusepa na ushindi wa mabao 3-0 na pointi tatu dhidi ya Mbao FC mchezo uliochezwa uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Nahodha wa Simba, John Bocco alianza kuitanguliza Simba dakika ya 24 kwa kichwa akimalizia pasi ya Mohamed Hussein aliyepiga mpira wa adhabu na Bocco kuuzamisha nyavuni kwa kichwa.

Kipindi cha pili kasi ya Mbao ilikuwa kubwa wakitafuta bao la kusawazisha ila mambo yalikuwa magumu kwao kwani dakika ya 59 Simba walipata penalti baada ya Peter Mwangosi wa Mbao kuunawa mpira eneo la hatari mwamuzi akamua ipigwe penalti iliyozamishwa wavuni na Bocco.

Dakika ya 80 beki wa Mbao alimchezea rafu Meddie Kagere eneo la hatari na kusababisha mwamuzi kuamua iwe penalti iliyopigwa na Kagere mwenyewe na kuiandika Simba bao la tatu la ushindi.

Kwenye mchezo wa leo kila mfungaji kajiongezea idadi yake ya bao ambapo Bocco leo amefikisha bao la 11 na Kagere akifikisha bao la 14 kama jezi yake ya mgongoni huku Hussein akitoa pasi yake ya bao ya pili leo TPL.

Simba wanafikisha pointi 57 baada ya kucheza michezo 22 wakibakiza pointi mbili kuwafikia Azam FC walio nafasi ya pili wenye pointi 59 huku zikabaki pointi kumi kuwafikia vinara Yanga wenye pointi 67, Simba wamebakiwa na michezo sita mkononi kuwa sawa na Yanga na Azam ambao wamecheza michezo 28.

2 COMMENTS:

  1. Saleh jembe rudia tena Bado 10...ikiwa bado viporo 6...Yanga anazidiwa magoli ya kufunga na amefungwa magoli Mara 3 zaidi ya Simba!Hongereni Simba!

    ReplyDelete
  2. Leo Dida Kafanya Kazi Nzuri, Na Niyonzima Anazidi Kunoga; TP Karibuni Machinjioni Pale Taifa... Simba Tuna Waamini Mkiwa Home. Mpambane Kufa Na Kupona, Angalau Mshinde Goli 3 Na Kuzid.i Wadau Wa Simba Jitokezeni Kwa Wingi Pale Taifa Tuujaze Uwanja Na Kutoa Sapoti ,,,,,

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic