March 31, 2019


DAKIKA 90 za mchezo wa Ligi Kuu kati ya Simba na Mbao zimekamilika uwanja wa Jamhuri, Morogoro, kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.

John Bocco alianza kufunga bao la kuongoza kwa Simba dakika ya 24 akimalizia faulo iliyopigwa na Mohamed Hussein.

Bocco alipachika bao la pili kwa Simba kwa mkwaju wa penalti baada ya mchezaji wa Mbao FC, Peter Mwangosi kunawa mpira uliopigwa na Mzamiru Yassin dakika ya 58.

Meddie Kagere alipachika bao la tatu kwa Simba baada ya beki  wa Mbao kumchezea rafu Kagere eneo la hatari na mwamuzi kutoa penalti iliyopigwa na Kagere dakika ya 79.

Simba leo wameanzisha jeshi lao kamili huku mlinda mlango namba moja Aishi Manula akiwa ameanzia benchi akimtazama Deogratius Munish.

Mashabiki waliojitokeza ni wengi kuona namna timu zao zitakavyoonyesha umwamba leo huku Mbao wakiwa na kumbukumbu ya ushindi kwenye mchezo wao wa kwanza uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

6 COMMENTS:

  1. Niliwahi kumshauri kocha wa mbao kuwa kabla ya kutoa makali dhidi ya Simba kwanza waiyulize akina Lipuli na Ruvu Shooting waliotumia lugha kama hizo na nini kikawakuta. Huyu mnyama hatari msicheze nae

    ReplyDelete
  2. Kelvin Yondani Alisema: "Anaamini Yanga Itabeba Ubingwa Msimu Huu Kwa Sababu Simba Lazima Wateleze" Atasubiri Sana Mwishowe Itaonekana Ni Uwongo Simba Nguvu Moja Kazi Ipo Kwa Waliyo Mbele Yetu!

    ReplyDelete
  3. Kama Simba alisha zifunga Yanga na Azam basi kuja kupoteza mechi kwa timu nyengine labda itokezee hujuma au wao wenyewe Simba walewe na ushindi au kama anavyosema Magufuli wachezaji waanze kuvimba vichwa nakuanza kujiona wao babu kubwa waanze kuleta madharau kwa baadhi ya timu.

    ReplyDelete
  4. Changamoto ya watanzania wamejawa na ubishi tu,ukweli hawautaki daima,,,,jamani aminini kwa SIMBA hii ubingwa kwa yanga wausahau miaka mia,simba mbele kwa mbele,,,,watani wanachechemea.

    SIMBA hii labda waletewe man/barca ila sio vilabu vya mchangani kina yebo yebo.

    ReplyDelete
  5. Brother Haji kasema 10 yrs back to back.Watani mtasubiri sanaaaaaa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic