March 31, 2019


Simba leo Jumapili itakuwa ikisaka rekodi ili kuweza kupoteza machungu na kuaibishwa na Mbao FC mwanzoni mwa msimu baada ya kipigo wakiwa ugenini. Kocha wa Simba, Patrick Aussem amewatoa hofu mashabiki.

Simba na Mbao FC zitapambana katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ukiwa ni mchezo wa raundi ya pili ya Ligi Kuu Bara baada ya ule wa awali ambao walicheza CCM Kirumba, Simba kupigwa bao 1-0.

Katika mchezo huo, Simba atakuwa mwenyeji lakini atatumia Uwanja wa Jamhuri baada ya ule wa Taifa kufungwa ili kupisha marekebisho ambao unatarajiwa kutumika kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Vijana U-17.

Timu hizo zimekutana mara tano huku Simba ikiibuka na ushindi mara tatu na ushindi huo ugenini mara moja na kwenye uwanja wa nyumbani mara mbili huku ikipoteza mara moja tena ugenini msimu huu.

Simba na Mbao ni timu ambazo hazijawahi kukutana mwezi wa tatu lakini katika ushindi wa nyuma, wachezaji wa Simba ambao wameifunga mara nyingi zaidi ni Mzamiru Yassin (2), Emmanuel Okwi(2), na Shiza Kichuya (2) ambaye kwa sasa hayupo Simba. Hata hivyo mchezo huu utakuwa na ushindani mkubwa

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic