March 26, 2019


AS Vita Club 🇨🇩 Sasa Rasmi Imethibitisha kumuuza Mshambuliaji wao hatari, Jean-Marc Makusu Mundele kwenda klabu yq RS Berkane ya Ligi Kuu nchini Morocco 🇲🇦.

Mkongo huyo mwenye umri wa miaka 26 Sasa, amekubali kusaini mkataba wa miaka mitatu kuwatumikia wababe hao wa Morocco baada ya kukubali dau la Mshahara kwa mwezi, Dola 35,000 (Tshs 82m).

Na wakati huo huo Vita Club imepokea dau nono kwenye mauzo ya nyota huyo, euros laki 430,000 (Tshs 1b, 141m) ndio uhamisho wake umekamilika na atajiunga na timu yake mpya baada ya kumalizika kwa msimu

Makusu kafunga magoli zaidi ya 40 kwa mwaka wa 2018 akiwa na Mabingwa hao wa DR Congo.

Kabla ya usajili huo kukamilika, awali ilelezwa kuwa Makusu angesajiliwa na Yanga kutokana na kufurahishwa namna alivyocheza katika mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba

7 COMMENTS:

  1. Unatania.Angesajiliwa na Yanga!!Wacha utani .

    ReplyDelete
  2. Tafadhali acha utani bhana!usimfananishe Makusu Mundele na Haritier Makambo

    ReplyDelete
  3. hao yanga wanaotembeza bakuli mpaka wachezaji wao wanagoma kwa kutolipwa mishahara mbona mnaandika vitu visivyo na uhalisia

    ReplyDelete
  4. msitufanye mahawani.Huo mshahara wake wa mwezi unanua wachezaji sita Yanga.Waandishi wa habari acheni masihara

    ReplyDelete
  5. Yanga!😂😂😂😂😂😂

    ReplyDelete
  6. Vipi yanga wanabahatisha mchezaji wa dau la mamilioni na pia mshahara wa mamilioni mengi kwa kutegemea pesa za bakuli hivo hata mchezaji mwenyewe habahatishi na huku imekuwa migomo kwa kutokulipwa wachezaji ni jambo la kawaida kabisa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic