HARUNA Niyonzima kiungo wa Simba ambaye ni fundi wa kuuchezea mpira anavyotaka amesema kuwa kwa sasa bado moto wa kikosi cha Simba hautapoa mpaka kufikia malengo ambayo wamejiwekea kimataifa na kitaifa.
Niyonzima ambaye mkataba wake ndani ya Simba unaisha mwishoni mwa msimu huu amesema kuwa anaona Simba ikipiga hatua kwenye mashindano ya kimataifa pamoja na kuendeleza moto wake ndani ya Ligi Kuu Bara kwa sasa.
Niyonzima amesema kuwa kinachomfanya aamini kwamba kikosi chake kitafika mbali ni kutokana na mipango iliyopo ndani ya timu na ushirikiano kwa kila mchezaji.
"Kwa sasa wachezaji na viongozi wote wana furaha baada ya kutinga hatua ya robo fainali hii yote inatokana na ushirikiano uliopo ndani ya timu pamoja na nguvu ya mashabiki, hivyo bado moto wetu utazidi kuwa mkubwa.
"Malengo makubwa na mipango bora inatubeba kwa sasa hivyo nina imani tutaendelea kufanya vizuri kwa upande wa Ligi ya Mabingwa pamoja na ligi kuu bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kikubwa sapoti ya mashabiki na dua," amesema Niyonzima.
Simba inashika nafasi ya tatu kwenye ligi baada ya kucheza michezo 21 ikiwa imejikusanyia pointi 54 mchezo wake wa kwanza hatua ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa utakuwa Aprili 5 Uwanja wa Taifa dhidi ya TP Mazembe.
Kutoka Championi








0 COMMENTS:
Post a Comment