STRAIKA HATARI VITA ALIYETAJWA KUTUA YANGA ANUNULIWA MOROCCO
AS Vita Club 🇨🇩 Sasa Rasmi Imethibitisha kumuuza Mshambuliaji wao hatari, Jean-Marc Makusu Mundele kwenda klabu yq RS Berkane ya Ligi Kuu nchini Morocco 🇲🇦.
Mkongo huyo mwenye umri wa miaka 26 Sasa, amekubali kusaini mkataba wa miaka mitatu kuwatumikia wababe hao wa Morocco baada ya kukubali dau la Mshahara kwa mwezi, Dola 35,000 (Tshs 82m).
Na wakati huo huo Vita Club imepokea dau nono kwenye mauzo ya nyota huyo, euros laki 430,000 (Tshs 1b, 141m) ndio uhamisho wake umekamilika na atajiunga na timu yake mpya baada ya kumalizika kwa msimu
Makusu kafunga magoli zaidi ya 40 kwa mwaka wa 2018 akiwa na Mabingwa hao wa DR Congo.
Kabla ya usajili huo kukamilika, awali ilelezwa kuwa Makusu angesajiliwa na Yanga kutokana na kufurahishwa namna alivyocheza katika mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba








Unatania.Angesajiliwa na Yanga!!Wacha utani .
ReplyDeleteYanga?! Msituletee vituko hapa.
ReplyDeleteTafadhali acha utani bhana!usimfananishe Makusu Mundele na Haritier Makambo
ReplyDeletehao yanga wanaotembeza bakuli mpaka wachezaji wao wanagoma kwa kutolipwa mishahara mbona mnaandika vitu visivyo na uhalisia
ReplyDeletemsitufanye mahawani.Huo mshahara wake wa mwezi unanua wachezaji sita Yanga.Waandishi wa habari acheni masihara
ReplyDeleteYanga!😂😂😂😂😂😂
ReplyDeleteVipi yanga wanabahatisha mchezaji wa dau la mamilioni na pia mshahara wa mamilioni mengi kwa kutegemea pesa za bakuli hivo hata mchezaji mwenyewe habahatishi na huku imekuwa migomo kwa kutokulipwa wachezaji ni jambo la kawaida kabisa
ReplyDelete