March 25, 2019


Droo ya upangaji wa makundi ya fainali za #AFCON2019 inatarajiwa kufanyika Aprili 12 mwaka huu nchini Misri ambapo Tanzania imewekwa kwenye chungu cha nne ikiwa pamoja na mataifa ya Mauritania, Namibia, Kenya, Benin na Madagascar.

Vyungu hivyo vimepangwa kwa mujibu wa viwango vya soka vya CAF, ambapo makundi sita yanatarajiwa kuundwa, kila kundi likiwa na timu nne na timu zilizo kwenye chungu kimoja hazitakutana kwenye kundi moja.

Kati ya mataifa 24 yaliyofuzu fainali hizo, ni mataifa matatu ambayo yamefuzu kwa mara ya kwanza katika historia yake ambayo ni Burundi, Mauritania na Madagascar.

Hii ni mara ya kwanza kwa Afrika Mashariki kuingiza timu nne kwa wakati mmoja kwenye michuano hiyo, ambazo ni Tanzania, Uganda, Kenya na Burundi.


Je, ungependa Tanzania ipangwe kundi moja na timu zipi?

3 COMMENTS:

  1. duh mara paa kundi moja na Egypt Nigeria South Africa Tanzania duh hatari

    ReplyDelete
  2. Kwa kiasi fulani kuna makosa mengi sana yamefanyika kuiandaa timu yetu ya taifa kwa ajili ya AFCON. Labda usimba na uyanga ndio unaotutesa? Kweli Simba kama klabu haiwezi kuwa timu ya taifa. Lakini Simba Kama klabu yenye ushindani wa ndani na michuano ya Africa ndio ilikuwa mahali sahihi pa kuanzia matayarisho yetu ya timu yetu kwa ajili ya AFCON. Kweli jitihada zinafanyika kuisapoti Simba kufanya vizuri klabu bingwa Africa ila wahusika wanashindwa kwenda kwa undani zaidi kuekeza kwa wachezaji wazawa wa Simba ikiwezekana kuwahamasisha kupambana ili wapate namba kucheza klabu Africa kwenye nafasi zao ili wawe msingi wa timu yetu ya taifa kwa mashindano ya AFCON yajayo. Tanzania ni miongoni mwa nchi chache zilizoingiza timu kwenye timu nane bora Africa. Tumechelewa lakini bado nafasi ipo kama Taifa ya kuwatumia wachezaji wa Simba kama msingi wa maadalizi ya timu ya Taifa. Tunachotakiwa kufanya watanzania hivi sasa ni kuiwezesha Simba kusonga mbele zaidi ya robo fainali ili wachezaji wetu wazawa ndani ya Simba wazidi kufaidika na changamoto za mechi kubwa Africa hakika watakuja kuleta mchango mkubwa ndani ya timu yetu ya Taifa. Nadhani hata waganda wanaiombea Simba kusonga mbele zaidi klabu bingwa Africa kwa kutegemea wachezaji wao wa taifa ndani ya Simba wazidi kupata ushindani wa mechi kubwa zaidi Africa iliwajekuwa msaada kwa timu yao Taifa kwa ajili ya AFCON. Kwa hivyo Kama taifa hatuna budi kutumia nafasi ya Simba kupika wachezaji wa Taifa stars pia.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic