March 28, 2019


KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, anakuna kichwa juu ya mbinu gani atumie wakati kikosi hicho kikiwa kinacheza katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro baada ya kusema wazi uwanja huo ni mbovu na hauendani na staili wanayocheza.

Simba wamelazimika kuhamia huko baada ya Uwanja wa Taifa waliokuwa wanautumia kupigwa kufuli kwa ajili ya matengenezo kabla ya Afcon ya vijana.

“Ndiyo tunaweza kuathirika kwa namna fulani kwa sababu pale Taifa sehemu ya kuchezea ni safi tofauti na Morogoro ambapo tunaenda kucheza kwa sasa.

“Tunahama kutoka sehemu nzuri na kwenda pasipo pazuri. Pale sehemu yake ya kuchezea wala siyo rafiki sana, kucheza pale inabidi tujiandae sana bila ya hivyo inaweza kutukwamisha na kushindwa kupata ushindi,” alimaliza kocha huyo aliyejenga imani kwa mashabiki wa Simba.

5 COMMENTS:

  1. Kwani hamjajuwa tokea mwanzo kuwa kiwanja kibovu au mlilazimishwa. Kwani ilikuwa hakuna jengine ni nyie wenyewe mloochaguwa na aasa mnalalamika nini?

    ReplyDelete
  2. UWANJA WA AMAN ZANZIBAR NDIO CHAGUO SAHIHI LA SIMBA KWA UWANJA WA NYUMBANI WA MDA. TENA HATA HALI YA HEWA HAZIPISHANI NA ILE YA DAR-ES-SALAAM. NADHANI HAPA HAKUKUWA NA USHIRIKISHWAJI WA BENCHI LA UFUNDI, VIONGOZI WAMETOA TU MAAMUZI WENYEWE.

    ReplyDelete
  3. LA SIVYO HATA PEMBA KULE PIA WANA UWANJA MZURI SANA.

    ReplyDelete
  4. si wanaruhusiwa kubadilisha

    ReplyDelete
  5. Huo uwanja ni mbovu na unaweza kuathiri harakati za kutetea ubingwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic