March 31, 2019


MENEJA wa Mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere, Patrick Gakumba anatua nchini hivi karibuni kukutana na viongozi wa Simba kuhusu dili ya nne tofauti. Kwa mujibu wa meneja huyo Raja Casablanca ya Morocco, Zamalek ya Misri, TP Mazembe na SC Vita zote za DR Congo zimefika bei kwa Kagere.

“Simba ndio wanashikilia mkataba wa Kagere kwa sasa, siwezi kuweka wazi kitu chochote hadi nitakapokutana na uongozi wa klabu hiyo ili niweze kuzungumza nao na ninatarajia kuja Dar hivi karibuni ndio nitajua kama atabaki ama la.

“Kuna timu nyingi ambazo zinamuhitaji Kagere ambazo ni TP Mazembe, SC Vita, Casablanca na Zamaleki zote hizo zilimfuata na kumtaka lakini hatujafikia makubaliano nazo.

“Kitaaluma na kibiashara watu wanakwenda kimkataba, Kagere ni mchezaji wangu ninammeneji lakini Simba ndio wenye mamlaka naye kwa sasa na ndio wenye maamuzi ya kumtoa ama la, hadi tukutane tukae na tuzungumze niwaombe ndipo nitakapowatangazia.

“Watu wakae watambue kwamba, Simba sasa hivi sio timu ya kawaida, maana imeingia katika timu nane bora za Afrika, maana ukiingia katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika hata dunia inakutambua, hata hivyo katika hatua ambayo imefikia hawawezi kumuachia mchezaji mzuri japokuwa lolote linaweza kufanyika,”aliongeza Gakumba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic