March 2, 2019



WAZIRI Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Edward Lowassa ambaye anapenda michezo ila ni msiri kuzungumzia timu anayoshabikia bongo, jana Ijumaa alitangaza kurejea ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akitokea Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Lowassa ambaye alijiengua CCM mwaka 2015 baada ya jina lake kukatwa kwenye mchakato wa kuwania nafasi ya urais, alijiunga na CHADEMA mwaka huo na alipata nafasi ya kugombea nafasi ya urais kupitia chama hicho, alishindwa na mpinzani wake John Pombe Magufuli kutoka CCM.

Baada ya kurejea CCM, Lowassa amepokelewa na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli katika ofisi ndogo za chama hicho zilizopo Lumumba jijini Dar es Salaam.

Baada ya kupokelewa kwake jana Lowassa alisema kwa kifunpi sababua ya kurehea ndani ya CCM kwamba "Narejea nyumbani, nimerejea nyumbani, haitoshi CCM oyee," alisema Lowassa.

1 COMMENTS:

  1. Hili ni jinamizi jengine kwa upande wa upinzani hasa Chadema ingawa wao wenyewe tayari wameshaanza kutoa kauli za kejeli kuhusiana na Lowasa kurudi CCM. Hakuna ubishi Lowasa alikipa ujiko ama boost Chadema na upinzani. Unaona kabisa hivi sasa kwa jinsi gani kurejea kwa Lowasa CCM kiti cha ubunge kwa mtu kama Lema pale Arusha kinavyoyumba. Uondokaji wa Lowasa kutoka chadema kutapelekea kupoteza baadhi ya wabunge vile vile kutoka upinzani,it is a just matter of time. Jambo moja kubwa la kujiuliza hivi sasa ni kwamba wapinzani hasa Chadema watampaka rangi gani ya kisiasa Lowasa baada ya kuwabwaga
    kwani wakati Lowasa akiwa CCM wapinzani walimpaka rangi ya ubadhirifu na walienda mbali zaidi kwa kusema kuwa kama wakikamata serikali basi Lowasa angeozea gerezani. Na nadhani kwa vitisho na mkwala huo wa upinzani ndipo CCM wakaona isiwe shida na kuamua kuliengua jina la Lowasa katika kinyan'ganyiro cha kugombea uraisi kwenye uchaguzi mkuu uliopita kitu kilichopelaka ghadhabu ama hasira kwenye moyo wa Lowasa na kuamua kuachana na CCM na kwa mshangao wa wengi wa watu walishuhudia Lowasa akipokelewa na Chadema kama Shujaa na kuanzia hapo upinzani nchini uliendelea kumpaka Muheshimiwa Lowasa rangi ya ushujaa uliotukuka. Yote katika mambo mengi ya siasa za upinzani nchini hasa kuhusiana na kisa kizima cha Lowasa inaonesha dhahiri kuwa wapinzani ni wanafiki na hakika kwa kiasi kikubwa wao ndio wafifishaji wakubwa wa ukuaji wa Demokrasia ya kweli nchini na kuetendelea kupandikiza fikra tata ndani ya mioyo mingi ya watanzania kuhusiana na hali ya siasa Tanzania. Kwa kuendelea kuishi kwangu nje ya Tanzania na kufuatilia hali za siasa za huku nje kwa ukaribu nilichojifunza ni kwamba upinzani nchini Tanzania walipoteza au waliwapotezea watanzania nafasi hadimu ya kujenga demokrasia ya kweli kwa kitendo chao cha kuamua kumpiga vita Magufuli from day one of his presidency. Kiuhalisia Magufuli hakuwa anashikamana na siasa za chama chochote bali alikuwa ni Nationalist au Mtaifa,kiongozi ambae anatunguliza maslahi ya nchi yake kwanza na kawaida ya aina ya kiongozi mwenye sifa ya utaifa kwanza huwa wapo tayari kufanya kazi na taasisi yoyote itakayoweka maslahi ya Taifa lao kwanza.kwa chadema na upinzani kuamua kumpiga vita Magufuli wakati wao kwa kipindi kirefu wakihuburi kukosekana kwa kiongozi mzalendo wa kweli nchini ni jambo la kushangaza sana na imedhihirisha yakwamba upinzani nchini Tanzania haupo vitani kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania bali wapo vitani kwa ajili kupigania madaraka yao binafsi hata kama nchi itaendeshwa na watu wa hovyo. Kwani kwenye Demokrasia ya kweli mtu akifanya vibaya una haki ya wazi ya kukosoa bila ya hofu lakini sio kwa chuki ili muhusika ajishahihishe kwani anaekukosoa mara nyingi huwa anakupenda.Na mtu akifanya vizuri basi unapompongeza vile vile bila ya chenga wala figisu ni haki yake ili kumpa morali ya kuendelea kufanya vyema zaidi. Lakini kwa upinzani nchini kutokuona au kupongeza hata moja zuri tangu serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani nadhani ni ndio chanzo kikubwa cha kuendeleza siasa za uadui nchini na kamwe wapinzani hawana jeuri ya kusema yakuwa serikali iliopo madarakani inawajengea mazingira ghasi ya kisiasa nchini bali ni wao wapinzani ndio walioanzisha na ndio wanaoendeleza siasa za chuki Tanzania hilo halina ubishi na si dhani kama aina hiyo ya siasa bado ina kiki miongoni mwa wa watanzania kwani mazingira ya siasa wakati wa kikwete na Magufuli yamebadilika kwa kasi ya ajabu ni vizuri wapinzani wakabadilika pia ili kuendana na mahitaji ya kisiasa ya wakati huu. Ushauri ni kwamba Tanzania ni nchi huru ya kisiasa hahihitaji tena ukombozi wa kisiasa. Na wanasiasa hasa wale wa upinzani waachane kabisa na kasumba hiyo ya kuwapumbaza watanzania kuwa wanahitaji kukombolewa kikisiasa. Kinachohitaji kukombolewa Tanzania ni hali za maisha za mtanzania kuwa bora zaidi ya sasa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic