March 10, 2019


YANGA wanadhidhirisha kwamba ukubwa dawa kwani licha ya kufungwa mapema dakika ya 16 na mshambuliaji wa KMC, Rashid Mohamed walinyanyuka na kuendeleza moto wao kwenye ligi kwa kuwatungua mabao 2-1 wapinzani hao mchezo uliochezwa leo Uwanja wa Taifa.

Bao la Yanga lilipachikwa na Papy Tshishimbi dakika ya 37 baada ya Deus Kaseke kupiga kona fupi iliyotua miguuni mwa Deus Kaseke kabla ya kupiga pasi iliyomkuta Tshishimbi na kufunga bao safi la kichwa.

Mpaka mapumziko timu zote zilikuwa zimetoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 hali iliyowafanya KMC waamini kwamba watarejea na pointi moja kutoka kwa vinara wa ligi kwa sasa Yanga ambao wana pointi 70.

KMC waliongeza moto wa mashambulizi kipindi cha pili ambapo kocha wa KMC Ettiene Ndirayagije alianza kwa  mabadiliko kwa kumtoa mlinda mlango Jonathan Nahimana nafasi yake ikachukuliwa na Juma Kaseja.

Dakika ya 62 Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera alifanya mabadiliko ya kiufundi kwa kumtoa Deus Kaseka akaingia Ibrahim Ajibu na Thaban Kamusoko nafasi yake ikachukuliwa na Amiss Tambwe.

Mabadiliko hayo yalileta matokokeo chanya kwani dakika ya 67 Ibrahim Ajibu alipiga pasi moja kumtamfuta Tambwe iliyomaliziwa na beki wa KMC Ally Ally ambaye alijifunga kwa kichwa safi kilichomshinda Kaseja wakati akiokoa mpira.

Baada ya bao hilo Kaseja alinyanyuka kishujaa na kumnyanyua All Ally ambaye alikuwa amekata tamaa baada ya kufunga bao lililodumu mpaka dakika 90 zinakamilika.

3 COMMENTS:

  1. Alinyanyuka kishujaa baada ya kufungisha timu.Au ndio yale yale ya kuongea na wachezaji?
    Ally Ally huyu huyu alifanya faulo dakika ya 89 mechi iliyopita nä kusababisha goli la Feisal Toto.
    Coincidence????

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hata JS Soura waliongea na Bukaba akawapa goli la Kwanzaa na kutoa penati

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic