March 28, 2019

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa wanatambua mchezo wao dhidi ya Alliance utakuwa mgumu ila watapambana kupata matokeo chanya yatakayowapa nafasi kusonga mbele hatua ya nusu fainali.

Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema wachezaji wana morali kubwa ya kupambana na wapo tayari kwa ajili ya mchezo hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi jumamosi Uwanja wa CCM Kirumba.

"Tupo tayari kwa mapambano kwa ajili ya mchezo wetu na wachezaji wana morali kubwa ili kupata matokeo, hesabu zetu ni kuona tunashinda ili tusonge mbele.

"Alliance ni timu nzuri kwa kuwa ina vijana wengi pia tumecheza nao michezo ya ligi hivyo tunawatambua vizuri, imani yetu ni kupata matokeo ili kusonga mbele kwa sasa tunahitaji sapoti ya mashabiki," amesema Saleh.

Yanga wakishinda mchezo wa Jumamosi watakutana na Lipuli hatua ya nusu fainali uwanja wa Samora hata Alliance pia nao wakishinda watamenyana na Lipuli ambayo jana ilipenya hatua ya nusu fainali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic