March 27, 2019


Klabu ya Yanga imepigwa faini ya shilingi milioni sita ( 6,000,000 ) kwa makosa mawili wakati wa mechi yao na KMC iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kosa la kwanza ilikuwa ni kupita mlango tofauti kuingia uwanjani.

La pili ni wakati wa mapumziko kutoingia katika vyumba maalumu vya kubadilishia nguo.

Kiasi cha shilingi za kitanzania milioni sita kutozwa Yanga zimetokana na kila kosa kugharimu milioni 3.

Baada ya faini hiyo, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Steven Mnguto, amesema udhaifu wa kanuni hizi watazifanya kuwa kali zaidi msimu ujao kwa kuziboresha.

Mwenyekiti ameeleza wataziboresha ili kuepuka kujirudia kwa matukio haya ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara.


1 COMMENTS:

  1. ni vyema wakiwa wanalipa pia mtujuze maana kanuni zipo wazi kwa wakaidi lakini hatuskii lolote kati ya hayo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic