March 27, 2019

 TIMU ya Barcelona ya kwa Mnyamani leo imekabidhiwa zawadi ya Kombe, Medali na vin'gamuzi vya Azam baada ya kuibuka na ushindi kwenye michuano ya El Clasico iliyochezwa Uwanja wa JMK Park dhidi ya Real Madrid.

Barcolona ya kwa Myamani iliibuka kidedea kwenye fainali hizo baada ya kuitungua Real Madrid bao 1-0 mchezo wa fainali uliochezwa hivi karibuni.

Mwakilishi wa La liga, Luis Cardenas amesema kuwa anaona fahari namna vijana wanavyopambana na kupata matokeo hali ambayo inazidi kuongeza mahusiano mazuri.

"Nina furaha sana kuona haya yakitokea kuna mengi sana ambayo yapo ila ni jambo la kufurahia namna watu walivyo na nia njema ya kupambana na kucheza, ujuzi ambao wanaupata unatupa nguvu na ninaona fahari kuona timu zikiwa zinapambana na mwisho wa siku mshindi anapatikana.

"Haikuwa rahisi kutimia hivyo wanapaswa pongezi, utayari wao umewasaidia waweze kufika hatua ya ushindi," amesema Cardenas.

Zawadi ambazo wamepewa washindi hao ambao ni Barcelona Kwa Mnayamani ni pamoja na kombe la El Clasico, Vingamuzi vya Azam, medali, dishi na jezi za Barcelona Orijino.

Naye Abdul Mohamed ambaye ni Meneja masoko wa Azam amesema kuwa mpango huu ni endelevu kutokana na sapoti ambayo wanaipata kutoka kwa La Liga na mashabiki wa Tanzania wanaopenda michezo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic