March 30, 2019


BEKI kitasa mkongwe wa Yanga, Kelvin Yondani amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo watakapowavaa wapinzani wao Alliance FC, katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho (FA).

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana leo kwenye Uwanja  wa CCM Kirumba mkoani Mwanza, mchezo unaotarajiwa kujaa upinzani mkubwa.

Huo ni mchezo wa pili timu hizo kukutana kwenye uwanja huo na mechi yao ya kwanza kucheza ilikuwa ya Ligi Kuu Bara ambayo ilimalizika kwa Yanga kushinda bao 1-0 lililofungwa na Mrundi, Amissi Tambwe aliyetokea benchi
kuchukua nafasi ya Deus Kaseke.

Yondani alisema anafahamu ubora wa kikosi cha Alliance, lakini hana hofu ya kupata ushindi katika mchezo huo. Yondani alisema, katika msimu huu wamepanga kuchukua mataji yote wanayoyashindania ubingwa ukiwemo wa ligi na Kombe la Shirikisho linaloshikiliwa na Mtibwa Sugar ambao wameondolewa tayari katika mashindano hayo.

“Tumeanza maandalizi ya mchezo dhidi ya Alliance muda mrefu na hiyo yote katika kukiimarisha kikosi chetu ili kuhakikisha tunapata ushindi na kutimiza malengo yetu.

“Na hili linawezekana kabisa kutokana na ubora wa kikosi chetu kinachoundwa na mchanganyiko wa vijana na wakongwe, licha ya kufahamu mchezo huo ni mgumu kwa pande zote mbili. “Lakini, licha ya ugumu wa pambano hilo niwaondoe hofu Wanayanga kuwa tunawapiga tena kwa mara ya pili nyumbani kwao,”alisema Yondani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic