UONGOZI wa Alliance FC umesema kuwa hauna hofu na kikosi cha Simba leo wana imani ya kuwafunga mabao mengi yatakayowapa nafasi ya kukaa sehemu nzuri kwenye ligi ambayo kwa sasa ushindani umezidi kuwa mkali.
Ofisa Habari wa Alliance FC, Jackson Mwafulango amesema kuwa ana imani na maandalizi ya kikosi waliyoyafanya, leo wanaingia uwanjani wakiwa kifua mbele tayari kumchinja mnyama bila huruma.
"Tuna kikosi kipana na chenye uwezo wa kupambana uwanjani, kama ambavyo ilikuwa kwenye mchezo wetu dhidi ya Yanga tulionyesha uwezo na mchezo mkali ila tulishindwa kwa changamoto ya penalti.
"Sasa wao kwa sasa wanatamba wana mchezaji anayeitwa Chama basi sisi tuna nyota wetu anaitwa Mapinduzi hivyo ngoma ni droo tupo vizuri tunahitaji pointi tatu ni halali yetu kwa kuwa tupo nyumbani, uwanja wetu wa CCM Kirumba." amesema Mwafulango.
Mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa Taifa, Alliance ilikubali kupoteza kwa kufungwa mabao 5-1, hivyo leo ni mzunguko wa pili mchezo utakaochezwa saa 10:00 Jioni.

0 COMMENTS:
Post a Comment