April 23, 2019


EMMANUELI Okwi, mshambuliaji wa Simba ambaye ni raia wa Uganda amefanikiwa kufunga bao baada ya kupita muda wa dakika 990 kwa kufunga bao uwanja wa Kaitaba wakati Simba ikipoteza kwa kuchapwa mabao 2-1.
Okwi ambaye alikuwa ni mfungaji bora msimu wa mwaka 2017/18 akifikisha mabao 20 msimu huu amefikisha mabao 8.
Mara ya mwisho Okwi kufunga ilikuwa ni October 10 mwaka jana uwanja wa Taifa, ambapo Simba ilicheza na Ruvu Shooting na waliibuka na shindi wa mabao 5-0 huku yeye akitupia 'hat trick'.
Tangu October Okwi hakufumania nyavu kwenye ligi licha ya Simba kucheza michezo 11 ambayo ni sawa na dakika 990 na siku ambayo alifunga bao kwa mara ya mwisho mpaka alipoibuka Kaitaba zilikuwa zimepita siku 174.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic