April 24, 2019


IMEELEZWA kuwa kimya kingi cha Meneja wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kutokuwepo katika kikosi hicho, kinatokana na kukabiliwa na matatizo ya kifamilia.

Katika siku za hivi karibuni, Cannavaro amekuwa haonekani kikosini hapo pindi timu hiyo inapokuwa ikicheza mechi zake mbalimbali, huku wengine wakisema amefungashiwa virago.

Championi Ijumaa katika kutaka kupata ukweli wa jambo hilo, lilifuatilia na imeelezwa juu ya matatizo hayo ya kifamilia.

“Cannavaro hajafukuzwa isipokuwa ameomba ruhusa ya muda mrefu kuna matatizo yanamkabili, ndiyo maana amekuwa haonekani.

“Bado ana mkataba wa miaka miwili Yanga, hivyo siyo rahisi kukatishia mkataba wake na kama watu wanavyojua klabu haina fedha, hivyo kukatisha mkataba wa mtu ni lazima umlipe, uongozi umekubaliana naye kuhusu maombi yake ya ruhusa, bado ni meneja wa Yanga,” alisema mtoa taarifa.

Championi lilipomtafuta, Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten kulizungumzia suala hilo alisema suala la Cannavaro ni la kiuongozi zaidi na alipotafutwa mwenyewe beki huyo wa zamani azungumze suala lake, simu yake ilikuwa haipatikani.

CHANZO: CHAMPIONI

8 COMMENTS:

  1. Huyo kaondoka kutokana na kutolipwa chake

    ReplyDelete
    Replies
    1. kama huna uhakika na jambo ni bora kukaa kimya kuliko kuongea vitu usivyovielewa halafu ukaonekana mjinga......kwa taarifa yako ni kwamba hajaondoka mwenyewe bali kaondolewa.....wape taarifa na mazumbukuku wenzio wanaokurupukia mambo wasiyoyajua na yasiyowahusu.

      Delete
  2. Dismas ten ni mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano maana yake ni kiongozi, sasa anapojibu kuwa hilo ni suala la kiuongozi maana yake halimhusu. Hapo ndiyo ninaposhindwa kumuelewa mbona mengine anayatolea taarifa hata ya timu nyingine nje na yanga?

    ReplyDelete
  3. wewe ndo huelewi.....unakurupuka kama huyo mwenzio....kama hujui au huna uhakika na jambo ni bora kuuliza kuliko kuongea vitu usivyovijua.Kuwa mkuu wa kitengo cha mawasiliano sio kuwa kiongozi wa yanga,aliposema kuwa ni suala la kiuongozi alikuwa sahihi kwasababu unapoongelea safu ya uongozi wa yanga Ten hayumo na chochote anachokisema Ten kuhusu klabu anakisema baada ya kupata maelekezo ya viongozi wa yanga.....so wewe uliedhani Ten hajielewi,wewe ndo hujielewi unakurupuka tu.

    ReplyDelete
  4. Waandishi wa Habari nao! ina maana hawaelewi kiongozi mjua yote wa Yanga! Kwanini wasimtafute ZAPESA? Angewajibu kiuhakika yule, yule ndiye Mwenyewe bhana, anaongoza kila mahala. Mtafuteni jamani huyo ndiye ................

    ReplyDelete
  5. Dismas ten nafasi yake haitendei haki kabisa, kama vp Yanga watafute mbadala wake ni kama vile nafas iko wazi japo kivuli kinaonekana

    ReplyDelete
  6. ASIPOTAKA KUSEMA ILI ASAIDIWE HAKI ZAKE MWACHENI MWENYEWE MBONA ZAHERA KESHASEMA

    ReplyDelete
  7. Kama Meneja kakimbia njaa, tupambane vinginevyo wachezaji wazuri wengi watatukimbia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic