April 24, 2019

2 COMMENTS:

  1. Waziri Mwakyembe tunamuheshimu lakini maelezo au utetezi wake kuhusiana na Serengeti boys kufanya vibaya una kera sana na hauna mshiko na kwa kiasi kikubwa unatia kichefuchefu. Muheshimiwa waziri amekuwa akileta siasa zaidi kunako michezo wakati mchezo wa mpira ni kazi ya hadharani. Sina shaka hata kidogo matokeo haya mabaya ya Serengeti boys ukimuuliza mkuu wa nchi anaonaje kuhusiana na matokeo hayo hapana shaka atakwambia walicheza hovyo na ikiwezekana wahusika wawajibike au wawajibishwe. Unajua hii hali ya viongozi wetu kuchukulia poa kila tunapopigwa ndio iliyoifikisha pabaya Tanzania. Tunapigwa kunako riadha tunachukulia,tunapigwa kunako ngumi tunachukulia poa,tunapigwa kunako mpira tunachukulia poa sisi watanzania hatuna hata sehemu moja tunayofanya vizuri kunako michezo tumekuwa watu wa visingizio kila siku. Kama vijana waliahidiwa mamilioni ya pesa basi ilikuwa kazi ya benchi la ufundi kutumia umahiri wa kazi yao kuwawezesha vijana kwenda kukutana na mamilioni hayo na ilikuwa ni wakati wa vijana wetu kujitoa uwanjani kama wangepata mafunzo mazuri waliyoyaopata kutoka kwa walimu wao lakini wameshindwa. Katika timu ya Taifa hasa ya vijana haiwezekani ikakosa mtaalamu wa ulezi wa Ubongo kwa vijana yaani mwanasaikolojia wa kuwaweka sawa vijana kiakili .
    Ila Kilichoiponza timu yetu ya U17 ni uwezo mdogo wa kusakata kandanda zidi ya timu walizokutana nazo kwisha habari. Halafu kocha bado anang'ang'ania kuendelea kuifundisha timu hiyo? Labda hayo ndio matokeo ya yakuwa na mkurugenzi wa ufundi wa TTF aina ya kina Ame Kinje kwani alishafeli mara kadhaa lakini cha kushangaza kufeli kwake huko kumekuwa ndio kigezo cha kuaminiwa zaidi na TTF,to be honest shirikisho letu linalosimamia mpira wetu halipo sawa na wanatakiwa kurekibika la sivyo yajayo yatasikitisha zaidi.

    ReplyDelete
  2. HAYO NDIO MANENO YA BUSARA, WAHUSIKA WAJITATHMINI SASA NA SIYO BAADAYE!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic