April 20, 2019


KOCHA Mkuu wa Angola U 17, Pedro Goncalves amesema kuwa anaiombea dua mbaya timu ya Uganda ipoteze leo kwenye mchezo wake wa mwisho dhidi ya Nigeria utakaochezwa Uwanja wa Taifa kama ambavyo dua za timu ya Taifa ya Tanzania Serengeti Boys zilivyo.
Angola wapo kundi A wakiwa na pointi tatu sawa na Uganda ambao nafasi yao ya kufuzu inategemea matokeo ya mechi kati ya Nigeria na Uganda.
Goncalves amesema kuwa wanatambua ushindani uliopo kwa sasa na ni timu moja tu ambayo imefuzu michuano hiyo hivyo ili wao wapenye ni lazima Uganda ipoteze leo kwenye kundi lao.
"Tunaiombea Nigeria iifunge Uganda leo na kama hesabu hiyo ikikamilika sisi tunamalizana na wapinzani wetu Serengeti Boys kisha tunafuzu kwenye michuano hii.
"Uwezo tunao na nia tunayo ila kikubwa kwanza ni ushindi wa Nigeria ambao wakishinda watafikisha pointi tisa na sisi tukimpiga Serengeti Boys tutakuwa na pointi sita ambazo wapinzani wetu hawana," amesema. 
Kocha wa Serengeti Boys, Oscar Mirambo amesema kuwa leo watapambana kufa na kupona na wana imani ya kupata matokeo kwenye uwanja wao wa nyumbani.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic