April 20, 2019


KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa leo lazima amchinje mnyama nyumbani kwake kwenye mchezo utakaochezwa Uwanja wa Kaitaba.
Mexime amesema kuwa anawatambua wapinzani wake vizuri na kasi waliyonayo wala haimtishi anajiamini na atawachinja bila huruma na kubeba pointi tatu.
"Nimemaliza kila kitu kuhusu maandalizi ya timu yangu dhidi ya Simba, sijui kuhusu safu yao ya ushambuliaji ama ugumu wa beki wao hapa kwangu ni lazima niwachinje tu,".
 Najiamini na ninaweza kufanya vizuri hivyo baada ya dakika 90 nitaongea kuhusu ushindi na matokeo ambayo nitayapata mbele ya Simba," amesema Maxime.
Kagera Sugar wanaingia uwanjani leo wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao wa mwisho mbele ya Yanga, huku Simba wanaingia wakiwa na kumbukumbu ya ushindi mbele ya Coastal Union.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic