April 19, 2019



UONGOZI wa Kagera Sugar umesema kuwa umejiaandaa kuzima kasi ya Simba kwenye mbio za kutetea taji lao msimu huu kwa kuibuka kidedea kwenye mchezo wao wa ligi utakaochezwa Jumapili uwanja wa Kaitaba.
Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa wamejipanga kiasi cha kutosha kupata pointi tatu zitakazoiweka timu katika nafasi nzuri kwenye msimamo.
"Tunajua ushindani uliopo na mechi yetu haitakuwa nyepesi ila tupo tayari kuisimamisha Simba kwenye harakati za kusaka ubingwa ili nasi tujiweke sehemu nzuri kwani hatuna mwendelezo mzuri msimu huu.
"Kwa namna ligi ilivyo na timu zilivyopishana pointi chache tunajua tukishinda tunapanda kwa nafasi kadhaa, tunawaheshimu wapinzani kwani wamekuwa na mwenendo mzuri ila kwenye mpira kila kitu kinawezekana, mashabiki watupe sapoti," amesema Maxime.
Kagera Sugar imecheza michezo 32 kwenye ligi na imejikusanyia pointi 36 ikiwa nafasi ya 17 kwenye msimamo huku wapinzani wao Simba wakiwa nafasi ya tatu baada ya kucheza michezo 23na wana pointi 60

1 COMMENTS:

  1. Maan a kawaulize wengi waliotamka maneno kama hayo na nini kilichowafika

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic