April 23, 2019


HARUNA Niyonzima leo ametakata uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza baada ya kupachika bao lake la kwanza msimu huu akiwa na klabu yake ya Simba kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Alliance FC ambapo Simba imeibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Niyonzima alianza kucheka na nyavu dakika ya 20 baada ya kumalizia pasi ndefu aliyopewa na Mzamiru Yassin alioutuliza kifuani kabla ya kumalizia shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Alliance.

Baada ya bao hilo Alliance walishtuka na kuongeza ulinzi mkali kwenye lango lao huku wakifanya mashambulizi ya kushtukiza hali ambayo haikusaidia kuzaa matunda mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zilipokamilika.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Alliance wakibadili mbinu kuikabili Simba na hakukuwa na mabadiliko kwa vikosi vyote viwili zaidi ya yaliyofanywa na Alliance dakika ya 37 kwa kumtoa Richard John ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Hussein Javo ila bado milango ilikuwa migumu kwa timu zote mbili.


Mbelgiji wa Simba Patrick Aussems alifanya mabadiliko dakika ya 57 kwa kumtoa Hassan Dilunga nafasi yake ikachukuliwa na Clatous Chama pia dakika ya 62 Alliance walifanya mabadiliko mengine kwa kumtoa Michael Chinedu na nafasi yake ikachukulia na Bigirimana Blaise bado milango ikawa migumu.

Dakika ya 64 Adam Salamba alitolewa nje na nafasi yake ikachukuliwa na Emmanuel Okwi ambapo ilimbidi asubiri mpaka dakika 11 zipite kufunga bao la pili dakika ya 75 akimalizia pasi ya Nicholous Gyan. 

Okwi anafunga mabao 2 Kanda ya ziwa baada ya la kwanza kufunga mbele ya Kagera Sugar Simba ilipokubali kufungwa mabao 2-1 na leo mbele ya Alliance FC. 

Ushindi wa leo unaifanya Simba izidi kujiongezea pointi ikiwa nafasi ya 3 imecheza michezo 24 na ina pointi 63 huku Alliance FC wakibaki na pointi zao 37 baada ya kucheza michezo 33 wakiwa nafasi ya 16.

Ushindani ulikuwa mkubwa hali iliyofanya kuwe na kadi za njano kwa wachezaji leo ambapo kwa Simba nahodha John Bocco dk ya 37 baada ya kujibizana na mwamuzi alionyeshwa kadi huku kwa upande wa Alliance kadi za njano walionyeshwa Michael Chinedu, dk ya 28 na Joseph James dk ya 79. 

3 COMMENTS:

  1. Yupo fire konki apewe tu mkataba mpyaaa

    ReplyDelete
  2. Hongereni Simba hakuna kubweteka wachezaji jiandaeni kwa kituo kinachofuata.KMC ni wabishi na wakamiaji hasa.

    ReplyDelete
  3. Kiujumla kikosi cha jana cha Simba kinahitaji pongezi, wachezaji wamecheza mechi kwa kujituma kwelikweli. Hakika hii inaleta sasa maana ya kikosi kipana.

    Pia, kuna wzchezaji wamebadilika kabisa uchezaji wao, yaani wameongeza kujiamini na pia wameongeza stamina katika uchezaji, na vilevile wameongeza kiwango cha kumudu kukaba, sio kama zamani ambavyo walikuwa wakikabia macho, wakipoteza mpira wanatembea uwanjani; mfano wa wachezaji hao ni kama vile Nickoras Gyan, Asante Kwasi, Mlipili, Salamba, wachezaji hawa wameongeza kitu katika uchezaji wao, jana wamenifurahisha sana, kwani wamepelekea timu kucheza kwa kujituma sana mwanzo hadi mwisho kwa kuungana na wenzao ambao huanza mara nyingi kikosi cha kwanza ambao uchezaji wao ulishakuwa wa kujituma tangu mechi za kimataifa, hivyo ikafanya mzani wa timu uwe kati.

    Ushauri wangu mwingine kwa kocha ni kuhusu Mchezaji Mkude, kwakweli huyu jamaa kwasasa angepewa mazoezi maalumu kwanza ili aendane na kasi ya kikosi ya kwanza.

    Kwasababu ubora wake ule ambao binafsi naufahamu sio huu alionao, kiukweli ameporomoka, na sijui ni nini sababu, kwasababu namba ya kikosi cha kwanza anaipata kila mechi ukiondoa hii ya jana, lakini ni nini ambacho kinamfanya ashindwe kujiamini! Mimi naona kazi yake uwanjani kwasasa ni kukimbia-kimbia tu uwanjani. Kukaba hakabi, akipewa pasi nzuri na wenzake yeye anapoteza mpira au akifanikiwa kutoa pasi basi unakuta pasi hiyo haifiki kwa mlengwa.

    Naomba kocha amuandalie program maalumu na namba ya kikosi cha kwanza amuachie mchezaji mwingine kwani namba yake hata Haruna anaimudu, Kotei anaitendea haki, kiujumla Simba kuna viungo wengi sana. Apumzike kidogo ili arudishe utimamu wake. Maana baada ya skendo yake ya kutoroka kambini kwenda klabu, ndo kiwango kimeporomoka kabisa!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic