April 23, 2019



FT Alliance FC 0-2 Simba

Uwanja : CCM Kirumba


Goooool Emmanuel Okwi dk ya 75

Goooool Haruna Niyonzima dk ya 20

MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Alliance FC na Simba umemalizika kwa Simba kusepa na pointi tatu muhimu.

Haruna Niyonzima amekuwa mchezaji wa kwanza aliyeona lango la mpinzani katika pambano dakika ya 20 akimalizia pasi ya Mzamiru Yassin.

Kipindi cha kwanza Simba walianza kwa kushambulia kwa kasi huku Alliance wakilinda ngome yao na kushambulia kwa kushtukiza kwa dakika za mwanzo.

Bao la pili lilipachikwa na Okwi dakika ya 75 akimalizia pasi ya Gyan.

Mashabiki wengi walijitokeza kuona amshaamsha ndani ya uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

2 COMMENTS:

  1. Tunataka kmc awe ngazi kumpita azam

    ReplyDelete
  2. Kiujumla kikosi cha jana cha Simba kinahitaji pongezi, wachezaji wamecheza mechi kwa kujituma kwelikweli. Hakika hii inaleta sasa maana ya kikosi kipana.

    Pia, kuna wzchezaji wamebadilika kabisa uchezaji wao, yaani wameongeza kujiamini na pia wameongeza stamina katika uchezaji, na vilevile wameongeza kiwango cha kumudu kukaba, sio kama zamani ambavyo walikuwa wakikabia macho, wakipoteza mpira wanatembea uwanjani; mfano wa wachezaji hao ni kama vile Nickoras Gyan, Asante Kwasi, Mlipili, Salamba, wachezaji hawa wameongeza kitu katika uchezaji wao, jana wamenifurahisha sana, kwani wamepelekea timu kucheza kwa kujituma sana mwanzo hadi mwisho kwa kuungana na wenzao ambao huanza mara nyingi kikosi cha kwanza ambao uchezaji wao ulishakuwa wa kujituma tangu mechi za kimataifa, hivyo ikafanya mzani wa timu uwe kati.

    Ushauri wangu mwingine kwa kocha ni kuhusu Mchezaji Mkude, kwakweli huyu jamaa kwasasa angepewa mazoezi maalumu kwanza ili aendane na kasi ya kikosi ya kwanza.

    Kwasababu ubora wake ule ambao binafsi naufahamu sio huu alionao, kiukweli ameporomoka, na sijui ni nini sababu, kwasababu namba ya kikosi cha kwanza anaipata kila mechi ukiondoa hii ya jana, lakini ni nini ambacho kinamfanya ashindwe kujiamini! Mimi naona kazi yake uwanjani kwasasa ni kukimbia-kimbia tu uwanjani. Kukaba hakabi, akipewa pasi nzuri na wenzake yeye anapoteza mpira au akifanikiwa kutoa pasi basi unakuta pasi hiyo haifiki kwa mlengwa.

    Naomba kocha amuandalie program maalumu na namba ya kikosi cha kwanza amuachie mchezaji mwingine kwani namba yake hata Haruna anaimudu, Kotei anaitendea haki, kiujumla Simba kuna viungo wengi sana. Apumzike kidogo ili arudishe utimamu wake. Maana baada ya skendo yake ya kutoroka kambini kwenda klabu, ndo kiwango kimeporomoka kabisa!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic